Diamond Platnumz kumbe nae anapenda siasa, na ameweka wazi kuwa kama leo akiacha muziki atapenda sana kuwa waziri wa michezo kwa sababu kazi hiyo anaimudu na haiwezi kumshinda.
Alipohojiwa na D’jaro Arungu katika kipindi cha Papaso, Diamond Platnumz amesema “Kwa sasa hivi siasa bado ila nikiingia kwenye siasa baadaye akimaliza mheshimiwa Nape nachukua mimi kile cheo cha Waziri wa Michezo, Kile nakiweza kabisa kwa sababu mimi ukinimbia sijui kuhusu mpira, movie mimi naweza kabisa nikiwa Waziri, nikavifanya na vikawa na maendeleo. Ni kitu ambacho naweza siyo nasema nataka kuwa mbunge ila mimi nataka ile siku nimeacha kufanya muziki naingia kwenye siasa basi nakuwa Waziri wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuboresha vitu“.