Baada ya mwanadada Linah Sanga kusema anatamani kuzaa
na mwanaume mwenye sifa kama za Darassa, rapa huyo wa
wimbo ‘Kama Utanipenda’ amefunguka na kuzungumzia kauli
hiyo.
Darassa amesema anaheshimu mawazo ya mwanadada
huyo.
.
“Hiyo ni kauli yake, naheshimu mawazo yake. Nimefunzwa
kuheshimu maoni ya kila mtu, kwa hiyo sina la kuzungumza
zaidi ya hapo kwa sababu hizo ni issue za privacy za watu,”
Katika hatua nyingine Darassa amewataka mashabiki wake
wa muziki kukaa mkao wa kula wa ujio wa kazi yake mpya
ambayo ataiachia katikati ya mwezi huu.