Msanii wa Bongo Flava Nasib Abdul a.k.a
Diamondplatnumz amesema anaunga mkono
kitendo cha serikali kutangaza kwamba kwa watu
wanaotumia plate number za majina yao
watatozwa milioni 10 kama kodi kutoka 5 kuanzia
mwaka wa fedha 2016 & 2017.
Kufuatia hotuba ya serikali kuonyesha hivyo
kipindi cha EADRIVE kinachorushwa na EA Radio
kimeongea na msanii #DiamondPlatnumz kuhusu
mkakati huo ikiwa yeye ni mmoja wa
wanaolengwa na jambo hilo.
Diamond anasema ‘’ Kama serikali itatumia fedha
hizo kusaidia watu wa hali ya chini mimi naona
sawa tuu’’