Simba SC watangaza zawadi kwa mashabiki 10,000 Simba Day

Simba SC wakishirikiana na Blueberry Travel Tanzania wametangaza zawadi kwa mashabiki 10,000 wakwanza kufika uwanjani. Mashabiki hao watapatiwa fomu ambazo watazijaza na kisha kuchezeshwa kwenye droo itakayosimamiwa na Blueberry Travel Tanzania kisha washindi watatu (3) watatangazwa kupitia kurasa rasmi za Simba SC.

Zawadi kwa Mshindi wa kwanza atapata nafasi ya kutembelea Dubai, huku mshindi wa pili atapata nafasi ya kuchagua kwenda nchi yoyote Afrika Mashariki, na mshindi wa tatu atapata atakatiwa tiketi ya ndege kwenda mkoa wowote ndani ya Tanzania.

Pia wamesisitiza hamna gharama yoyote ya kujaza fomu hizo.

Simba Day

Pata Update zaidi kupitia page yetu ya facebook Hassbaby Mapacha

Kwa habari zaidi za Michezo bonyeza HAPA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *